Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA

Mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran yaanza tena hii leo nchini Iran

Mazungumzo ya siku mbili kuhusu mpango wa Nyukilia wa Iran yameanza tena hii leo mjini Geneva nchini Uswisi, huku pande zote zikieleza kuwa na matumaini ya kutapatikana kwa mafanikio. Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton ndiye Mwenyekiti wa mazungumzo hayo.

REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Pande zote zimesema hii ni hatua kubwa kufikiwa katika miaka ya hivi karibuni ingawa haitakuwa kazi rahisi kufikiwa kwa makubaliano yatakayoridhiwa na pande zote.

Mkutano huo unawakutanisha Maofisa wa serikali ya Iran na wawakilishi toka Marekani, Uingereza, China, Ufaransa, Urusi na Ujerumani.

Mkutano huu ni wa pili toka Rais wa sasa wa Iran, Hassan Rouhani aingie madarakani mwezi Agosti mwaka huu.

Kwa pamoja wajumbe wanatarajiwa kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na Iran kuhusu mpango wake wa matumizi ya Nyuklia.

Mapendekezo hayo yamekuwa yakikosolewa na Israel inayotaka mataifa ya Magharibi kutolegeza vikwazo vyao dhidi ya Tehran mpaka pale itakapojiridhisha kuwa mpango huo si hatari kwa usalama.

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakiishuku Iran huenda inatafuta uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia kupitia mpango wake huo lakini Taifa hilo limekuwa likikanusha na kusema kuwa lengo lao ni matumizi salama pakee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.