Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-URUSI

William Hague asema Mazungumzo ya amani Syria yahusishe makundi yenye msimamo wa kati

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague amesema mazungumzo ya amani ya Syria ni lazima yahusishe makundi yenye msimamo wa kati,kiongozi huyo ameyasema hayo katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa ya kiarabu na yale ya magharibi yalipokutana na wawakilishi wa upinzani wa Syria.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza,William Hague
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza,William Hague Reuters/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya London Uingereza yanajaribu kuandaa mazingira mazuri ya mazungumzo ya amani yatakayofanyikia huko Geneva mwezi ujao.

Hata hivyo Kundi kuu la Upinzani nchini Syria limetishia kugomea mktano wa pili wa Geneva.

Baraza la taifa la Syria SNC limeshindwa kufanya mazungumzo na wajumbe wa serikali ya raisi Bashar Al Assad.

Mawaziri hao wanataraji kuonesha msisitizo juu ya umuhimu wa makundi yote hasimu nchini Syria kukutana katika meza moja kwa mazungumzo ili kufanikisha mpango wa amani wa taifa hilo.

Mataifa ya Uingereza,Misri,Ufaransa,Ujerumani,Jordan,Italia,Qatar,Saudi Arabia,Uturuki,Falme za kiarabu na Marekani zinatarajiwa kurejelea maoni kuhusu mkutano wa pili wa Geneva unapaswa kujadili mageuzi ya kisiasa na kinyume na utawala wa Assad.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.