Pata taarifa kuu
URUSI-ISRAEL-IRAN-EU

Matumaini yafufuka katika mazungumzo ya Uswisi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran

 Mazungumzo kati ya mataifa ya magharibi na ujumbe wa Iran yanaingia siku yake ya pili hii leo huku kukiwa na matumaini kuwa huenda safari hii mazungumzo haya yakazaa matunda licha ya ugumu uliopo.

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton
Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton REUTERS/Mohamed Abd El
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanayofanyika mjini Giniva Uswis na kusimamiwa na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton ambaye kupitia msemaji wake anasema kuna matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano kuhusu baadhi ya mapendekezo kuhusu mapngo wa nyukilia wa Iran.

Kwa upande wake nchi ya Iran kupitia kwa naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Abbass Aragachi anasema kuwa nchi yake haikuja kwenye mazungumzo haya kama watalii na kwamba wamejidhatiti kushirikiana na jumuiya ya kimataifa huku akishindwa kueleza undani wa mapendekezo yao mapya.

Viongozi kutoka Mataifa yenye nguvu duniani kwa siku ya pili wamekuwa na mazungumzo mjini Geneva Uswis juu ya nchi ya Iran kuhusu mpango wake wa Nyuklia,Mazungumzo haya ya siku mbili yanatarajiwa kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa na nchi ya Iran kuhusu mpango wke wa nyuklia na namna inavyopanga kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.

Mazungumzo ambayo yanalenga kumaliza tofauti kati ya Iran na jumuiya ya kimataifa jkuhusu mpango wake wa Nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.