Pata taarifa kuu
KENYA

Wakuu wa Usalama wa Taifa Nchini Kenya waanza kuhojiwa juu ya mkasa wa kigaidi kwenye Jumba la Biashara la Westgate

Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mambo ya Nje inatarajiwa kuanza kibarua cha kuwahoji Viongozi Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa juu ya mkasa wa shambulizi la kigaidi uliotekelezwa kwenye Jumba la Biashara la Westgate uliochangia vifo vya watu sitini na saba.

Polisi waliokuwepo kwenye shambulizi la kigaidi la Jumba la Biashara la Westgate kupambana na wavamizi
Polisi waliokuwepo kwenye shambulizi la kigaidi la Jumba la Biashara la Westgate kupambana na wavamizi
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mambo ya Nje Asman Kamama amesema wataanza mahojiano hayo maalum kwa lengo la kutaka kujua wapi kumekuwa na uzembe uliochangia kushindwa kubainika kwa mpango huo wa kufanya shambulizi kwenye Jumba la Westgate.

Kamama na wajumbe wengine wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mambo ya Nje walitembelea eneo la Jumba la Biashara la Westgate kwa ajili ya kujionea madhara yaliyochangiwa na kutekelezwa kwa mkasa huo na wameonekana kusikitishwa sana na athari walizoziona.

Mahojiano hayo yanatarajiwa kuanza hii leo kipindi hiki kukiwa na taarifa ya kwamba kulikuwa na onyo lililotolewa zaidi ya mwaka mmoja uliopita juu ya kuandaliwa kwa shambulizi hilo la kigaidi la Westgate lakini hakukuwa na hatua zozote za haraka zilizochukuliwa katika kulidhibiti.

Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mambo ya Nje imekataa kuanza kunyosha kidole cha lwama kwa mtu yoyote kama alizembea kwenye shambulizi hilo la kigaidi lakini wamesisitiza uchunguzi watakaoufanya utabainisha kila kitu kilichotokea na kama kunawatu watapaswa kuwajibika.

Haya yanajiri kipidhi hiki Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya likitoa ripoti inayoonesha watu thelathini na tisa hawajulikani walipo tangu kutokea kwa mkasa wa shambulizi la kigaidi la Westgate na jamaa zao wameendelea kuwasaka bila ya mafanikio yoyote.

Serikali kuputia Waziri wa Usalama wa Ndani Joseph Ole Lenku ilitangaza hakuna maiti yoyote iliyokuwepo ndani ya Jumba la Biashara la Westgate na hivyo watu waliouawa ni sitini na saba pekee na wala hakuna mwili mwingine uliopatikana.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi Ndung'u Gethenji amesema kamati yao imetoa pendekezo la kufungwa kwa kambi zote za wakimbizi wa Somalia ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa nchi hiyo unaimalishwa.

Kenya imekuwa ikiwahifadhi zaidi ya wakimbizi laki tano kutoka Somalia ambao wamekimbia vita na umaskini na wamekuwa wakihifadhi huko Dadaab lakini wamekuwa wakituhumiwa kutumika kwenye mashambulizi yanayotekelezwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.