Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Tume ya haki za binadamu nchini Australia kuchunguza vitendo vya unyanyasaji wa wanawake

Serikali ya Waziri Mkuu wa Australia Julia Gillard leo Jumamosi imeiagiza tume ya haki za binadamu nchini humo,kuanza uchunguzi kuhusu vitendo wanavyotendewa wanawake wakiwa mahali pa kazi, ikiwa ni ishara ya kurejea kwa suala la usawa wa kijinsia.

Waziri mkuu wa Australia Julia Gillard
Waziri mkuu wa Australia Julia Gillard RFI
Matangazo ya kibiashara

Kamishina wa unyanyasaji wa Kijinsia Elizabeth Broderick atasimamia utafiti wa kitaifa wa kutathmini kiwango cha nyanyasaji, asili na matokeo ya unyanyasajii unaohusiana, hasa, katika suala la ujauzito kazini na baada kurudi kazini baada yalikizo ya uzazi.

Uchunguzi huo ataitisha mfululizo wa vikao vya majadiliano na wamiliki wa viwanda na makundi ya waajiri,vyama vya wafanyakazi, wafanyakazi na mashirika mengine kabla ya kuandaa mapendekezo ya kupunguza unyanyasaji.

Aidha mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Mark Dreyfus amesema kuwa upo ushahidi muhimu na wa kutosha kwamba wanawake wamekuwa wakifanyiwa unyanyasaji kwa kupunguzwa kazini, kufukuzwa ama uwajibikaji wao kutozingatia muda wa wao kuwepo kazini hasa baada ya kutoka katika likizo ya uzazi.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.