Pata taarifa kuu
MYANMAR

Vurugu mpya za kidini zaibuka nchini Myanmar wananchi waomba ulinzi zaidi

Kumeshuhudiwa vurugu mpya za kidini mashariki mwa nchi ya Myanmar kwa siku ya pili mfululizo wakati huu wananchi wa maeneo yaliyoathirika wakiomba msaada wa usalama toka kwa wanajeshi wa Serikali.  

Moja ya maeneo yaliyochomwa moto nchini humo kutokana na vurugu za kidini
Moja ya maeneo yaliyochomwa moto nchini humo kutokana na vurugu za kidini Reuters
Matangazo ya kibiashara

Jana usiku msikiti, kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na maduka vilichomwa moto kufuatia kuibuka mtafaruku wa kiitikadi kati ya waislamu na watu wa jamii ya Kibudha.

Vurugu hizo zimetokea kwenye jimbo la Shan ambapo usiku wa kuamkia leo watu wanaodhaniwa kuwa ni wajamii ya kibudha walivamia makazi ya watu na kuanza kuwasaka waumini wa Kiislamu ambao inawatuhumu kuwaua wafuasi wao.

Serikali ya nchi hiyo imetoa wito kwa wananchi kulinda usalama wao na kuachana na vurugu wakati huu ambapo mzozo huo unashughulikiwa ili kujaribu kumaliza tofauti za kidini ambazo zimeanza kukita mizizi nchini humo.

Kabla ya vurugu za leo, polisi walitoa tangazo kuhusu kufanikiwa kurejesha usalama kwenye mji huo lakini hali ilikuwa kinyume kwani haikuchukua muda kabla ya kuzuka kwa mapigano kati ya jamii hizo mbili.

Vurugu hizo zinzaelezwa kuzuka baada ya waumini wa Kiislamu kudaiwa kumuua mwanamke mmoja wa madhehebu ya Budha ambapo waumini wake walichukizwa na kitendo hicho na kutekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.