Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Upinzani nchini Venezuela walalama Chama Tawala kinatumia vibaya rasilimali za umma kuelekea Uchaguzi Mkuu

Upinzani nchini Venezuela umeanza kutoa kilio cha kuwepo kwa mbinu chafu zinazoweza kuchangia Uchaguzi Mkuu nchini huo kutokuwa huru na wa haki baada ya kugundua baadhi ya mbinu hizo kuanza kutumika.

Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Henrique Capriles amemlalamikia Kaimu Rais Nicolas Maduro kwa kutumia rasimali za umma kujijenga kuelekea Uchaguzi Mkuu
Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Henrique Capriles amemlalamikia Kaimu Rais Nicolas Maduro kwa kutumia rasimali za umma kujijenga kuelekea Uchaguzi Mkuu REUTERS/Tomas Bravo
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi Mkuu wa Upinzani Henrique Capriles amemtuhumu vikali Kaimu Rais wa Venezuela Nicolas Maduro kwa kutumia vibaya vyombo vya habari vya umma pamoja na fedha katika kampeni yake.

Kilio cha Capriles kimekuja kipindi hiki ambacho harakati za kampeni kwa ajili ya kurithi nafasi ya Kiongozi wa Taifa hilo Marehemu Kamanda Hugo Chavez zikiendelea kwa kuanza kwa kampeni za kusaka Urais.

Capriles amesema Kaimu Rais Maduro amekuwa akitumia vyombo vya habari vya umma vibaya kwa lengo la kueneza propaganda ili kuhakikisha tu wanauzoofisha upinzani nchini humo na Chama Tawala kuendelea kuongoza.

Upinzani umesema vitendo hivyo ambavyo vinafanywa na Kaimu Rais Maduro ni ishara ya wazi kabisa kampeni hazipo huru na hata uchaguzi nchini humo hautakuwa huru na wa haki kitu ambacho kitachangia kudumaza demokrasia.

Capriles ameoneaka mwenye hasira na kusema Maduro hakupaswa kutumia rasilimali za nchi kwenye mchakato wa kampeni za urais kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwadhulumu wananchi hao yao kikatiba.

Kampeni rasmi nchini Venezuela zinafunguliwa jumanne hii lakini Capriles amemtuhumu Maduro kutumia saa 46 kwenye Televisheni ya Taifa kujinadi tangu kutokea kwa kifo cha Kamanda Chavez tarehe 5 machi.

Capriles ametoa ujumbe mzito kwa Tume Huru ya Uchaguzi kuhakikisha inatenda haki kwa pande zote ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni ambazo zitakuwa za usawa na uchaguzi haki na huru hapo tarehe 14 April.

Waziri wa Mawasiliano Ernesto Villegas amejitokeza na kumjibu Capriles na kumwambia Televisheni ya Taifa imekuwa ikitangaza moja kwa moja mikutano yake na Waandishi wa Habari na wala hakusema anapendelewa.

Villegas amempa mwaliko Capriles kwenda katika Televisheni ya taifa kwa kufanyiwa mahojiano licha ya Kiongozi huyo wa Upinzani kukataa mwaliko aliopewa hapo awali.

Wananchi wa Venezuela wanalazimika kurejea kwenye uchaguzi mkuu ambao walifanya mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na Rais Mteule Marehemu Kamanda Chavez kufika na umauti baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.