Pata taarifa kuu
VENEZUELA-CUBA

Hali ya Afya ya Rais Chavez imeanza kuimarika akiendelea na matibabu nchini Cuba

Hali ya Afya ya Rais wa Venezuela Hugo Chavez imeanza kutengemaa tofauti na ilivyokuwa hapo awali na hizi zinakuwa taarifa njema za kwanza tangu afanyiwe upasuaji wa saratani nchini Cuba majumamatatu yaliyopita.

Picha ya Rais Hugo Chavez ikiwa imebebwa na mfuasi wake katika Jiji la Caracas huku wengi wakimuombea apone haraka
Picha ya Rais Hugo Chavez ikiwa imebebwa na mfuasi wake katika Jiji la Caracas huku wengi wakimuombea apone haraka ©Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa Rais Nicolas Maduro ndiye ametangaza kutengemaa kwa afya ya Rais Chavez ambaye anaendelea kupatiwa matibabu huko Havana na kusema amefanikiwa kuzungumza naye mara mbili katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

Maduro amekashifu vikali wale waote ambao wanaosambaza habari za uzushi juu ya hali ya afya ya rais Chavez na kusema Kiongozi huyo ameanza kurejea katika hali yake ya awali na kurejesha matumaini ya kuendelea na kazi zake.

Makamu wa Rais Maduro anatarajiwa kurejea Caracas hii leo baada ya kuridhishwa na hali ya afya ya Rais Chavez na ameowandoa hofu wananchi wa Venezuela na kuwaeleza muda si mrefu wataungana na Kiongozi wao.

Maduro amekiri kwa sasa Rais Chavez anatambua kila kitu ambacho kianendelea na hata namna ambavyo anaendelea kupata ahueni baada ya kufanyiwa upasuaji huko Havana na jopo mahiri la madaktari.

Makamu wa Rais Maduro ameongeza kwamba Rais Chavez ameendelea kusisitiza wananchi waendelea kupatiwa taarifa zake za ugonjwa kila mara na waelezwe ukweli pasi na kufichwa chcohote.

Rais Chavez ambaye aliibuka mshindi kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu nchini Venezuela mwezi Oktoba mwaka jana anatarajiwa kuapishwa tarehe kumi na mwezi huu lakini haijaelezwa kama atahudhuria sherehe hizo.

Chavez mwenye umri wa miaka hamsini na nane alianza kuongoza Venezuela mwaka elfu moja mia kenda tisini na tisa na ushindi wake wa mwezi Oktoba umemfanya apate fursa ya kikatoba kuongoza kwa kipindi cha nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.