Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SYRIA

Uingereza kuhamasisha mazungumzo na Uongozi wa upinzani wa Syria

Upinzani nchini syria huenda ukatambulika rasmi na taifa la uingereza baada ya kufanya maongezi jijini london,mkutano utakao wakutanisha viongozi wa uingereza na wa upinzani kutoka syria.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni wa uingereza Wilium Hague amethibitisha hayo na kuongeza kuwa amehamasisha Ahmed Moaz al Khatib na manaibu wake wawili ambao wapo katika ziara yao katika mji mkuu wa magharibi tangu kuundwa rasmi kwa upinzani wa Syria juma lililopita kwa hitaji la kuleta umoja na kutetea haki za binadamu.

Baada ya mkutano katika ofisi ya mambo ya kigeni waziri Hague alisema kuwa matumaini yameonekana katika muungano wa viongozi hao na anataraji kutoa taarifa bungeni juu ya suala hilo juma lijalo.

Mataifa kama Ufaransa na Uturuki yanautambua rasmi upinzani wa Syria kama kundi jipya nchini Syria na waziri Hague amesema kuwa Uingereza iko mbioni kufuata nyayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.