Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-GAZA

Israeli yasema iko tayari kusitisha mapigano yanayoendelea katika eneo la Ukanda wa Gaza

Serikali ya Israeli imesema ipo tayari kusitisha mapigano ambayo yanaendelea katika eneo la Ukanda wa Gaza kipindi hiki ambacho wamepeleka askari zaidi katika eneo hilo kukabiliana na Wapiganaji wa Kundi la Hamas.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Jerusalem imesema itaacha kutekeleza mashambulizi yake huko Ukanda wa Gaza punde tu Kundi la Hamas na Makundi mengine ya kigaidi yatakapositisha kurusha maroketi yao.

Kauli hiyo inakuja huku serikali ya Marekani kupitia Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Mark Toner ikiendelea kusisitiza mapigano ambayo yanaendelea Ukanda wa Gaza yamechangiwa na Kundi la Hamas.

Tonny Blair ambaye ni Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa UN katika Mashariki ya Kati kwa upande wake anaona hatua za muda mfupi zinazoweza kuchukuliwa na kwa pande zote kusitisha mashambulizi.

Tangu kuuawa kwa Kiongozi wa Kijeshi wa Kundi la Hamas Ahmed Jaabari kunaeleza kushuhudiwa kurushwa kwa maroketi zaidi ya mia tatu kutoka Palestina huku Jeshi la Israeli likijibu kwa kutumia ndege za kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.