Pata taarifa kuu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio kuhusu Syria siku moja tu baada ya msuluhishi Kofi Annan kutangaza kujiuzulu.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa linapiga kura ya kupitisha azimio dhidi ya serikali ya Syria siku moja tu baada ya msuluhishi wa mgogoro huo Koffi Annan kutangaza kujiuzulu. Annan amesema amelazimika kuchukua uamuzi huo kutokana na mpango wake wa amani wa kumaliza machafuiko nchini Syria kutotiliwa maanani na pia mataifa yenye nguvu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kushindwa kuwa na kauli moja hivyo kuifanya kazi yake kuwa ngumu.

Mapigano nchini Syria
Mapigano nchini Syria
Matangazo ya kibiashara

Mapigano makali yameripotiwa leo siku ya Ijumaa kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa jeshi huru la Syria katika miji mbalimbali ukiwemo mji mkuu Damascus na mji wa Aleppo ambapo ndege za jeshi la Syria limeshambuli ngome ya wapiganaji wa jeshi huru la Syria.

Jijini Damascus mapigano yameshuhudiwa katika kata ya Tandamoun kusini mwa mji mkuu karibu na kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Yarmouk ambako raia 21 wakiwemo watoto 2 wameuawa na kombora lililorushwa. Shirika linalo tetea haki za bindamu nchini Syria OSDH limesema takriban watu 179 wameuawa wakiwemo raia 110 katika maeneo mbalimbali ya mapambano.

Takwimu ya awali iliotolewa na OSDH ilisema raia 15 wameuawa katika mji wa Yarmouk.

Kiongozi wa OSDH Rami Abdel ameliambia shirika la habari la AFP kuwa hawajuwi kombora hilo lilirushwa katika kambi ya Yarmouk lilirushwa kutoka upande gani wa mapambano, na ameomba uchunguzi wa kimataifa uanzishwe.

Kambi ya Yarmouk inaorodhesha wakimbizi 148.000 wa Palestina waliopewa hifadhi nchini Syria ambao wote wanatambuliwa na Umoja wa Mataifa UN.

Upande mwingine, mashambulizi yameibuka mjini Damascus katika kata ya Jdeidet Artouz ambako mapigano yaliripotiwa karibu na uwanja wa ndege wa Marj el Sultane.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.