Pata taarifa kuu
Guinea- Bissau

Guinea Bissau kupiga kura za urais siku ya Jumapili

Kampeni za Uchaguzi zinamalizika hii leo nchini Guinea Bissau wakati Raia nchini humo wakijiandaa kupiga Kura kuchagua Rais atakayeliongoza Taifa hilo.

Aliyekuwa Rais wa Guinea-Bissau, Hayati Malam Bacai
Aliyekuwa Rais wa Guinea-Bissau, Hayati Malam Bacai timeslive.co.za
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ametoa wito wakuwepo kwa kura za Amani na uwazi wakati wote wa zoezi la kupiga Kura, zoezi litakalofanyika siku ya Jumapili
 

Kura hizo zimekuja baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Taifa la Guinea Bissau Malam Bacai Sanha kilichotokea mwezi Januari baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 

Wagombea tisa wanawania nafasi hiyo ya juu ndani ya Taifa hilo ambalo limekumbwa na misuguano kati ya Jeshi na Serikali ambayo imesababisha Nchi hiyo kuyumba.
 

Mbali na kuwa na kampeni za wiki tatu zilizofanyika kwa amani, baadhi ya Raia wana hofu kuwepo kwa Machafuko na Jeshi kuingilia Kati iwapo Jeshi la Nchi hiyo halitaafiki ushindi wa Mgombea yeyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.