Pata taarifa kuu
Pakistan

Pakistan yakasirishwa na shambulizi la wanajeshi wa NATO katika mpaka wake na Afganistan na kuwaua zaidi ya watu 20

Serikali ya Pakistan inataka uchunguzi wa haraka kufanyika kuhusu shambulizi lililofanywa na wanajeshi wa NATO,wakiongozwa na wale wa Marekani katika mpaka wake na Afganistan na kusababisha vifo vya watu 26 siku ya Jumamosi.

Malori ya wanajeshi ya NATO
Malori ya wanajeshi ya NATO REUTERS/Shahid Shinwari
Matangazo ya kibiashara

Kamati maalum ya usalama ,inayoongozwa na waziri Mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani imeamua kuwa, Pakistan sasa haitashirikiana na wanajeshi wa NATO nchini Afganistan.
 

NATO inasema shambulizi hilo huenda liliwauawa raia ambao huenda sio magaidi, katika mpaka wa Pakistan na Afganistan na msemaji wa oparesheni ya majeshi hayo,Jenerali Carsten Jacobson ameomba radhi na kutuma risala za rambirambi kwa serikali ya Pakistan na kusema kuwa uchunguzi unaendelea kubaini namna shambulizi hilo lilivyotekelezwa.
 

Nayo Marekani kupitia waziri wake wa Ulinzi Leon Panetta pamoja na waziri wa nchi za kigeni Bi.Hillary Clinton aidha wametuma risala zao za rambirambi kwa serikali ya Pakistan na kusema wanaunga mkono uchunguzi wa NATO ili kubaini namna shambulizi hilo lilivyotokea.
 

Marekani pia imesema kuwa,Pakistan ni mshirika wa karibu na wa maana sana katika vita dhidi ya magaidi wa Taliban na Al-Qaeda.
 

Zaidi ya wanajeshi wa NATO,Laki Moja wakiongozwa na wale kutoka Marekani wanaendeleza operesheni ya kupambana dhidi ya Taliban na Al-Qaeda katika mpaka wa Pakistan na Afganistan.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.