Pata taarifa kuu
Afghanistani

Wanajeshi 14 wa NATO wauawa mjini Kabul katika shambulio la kujitoa mhanga

Wanajeshi wawili wa vikosi vya NATO nchini Afghanistani wameuawa kusini mwa nchi hiyo na mtu alievalie sare za kijeshi jumamosi hii octoba 29 huku, askari wengine 14 wa NATO wengi wakiwa ni Wamarekani wameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga jijini Kaboul. Takriban raia wanne wa Afghanistani na polisi mmoja wameuawa pia. Kundi la Taliban limekiri kuhusika na mashambulizi hayo.

Wanajeshi 16 wa NATO wafariki katika shambulia la kujitowa muhanga
Wanajeshi 16 wa NATO wafariki katika shambulia la kujitowa muhanga REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari lililobeba mabomu alivizia msafara wa wanajeshi wa NATO kusini magharibi mwa mji mkuu Kaboul na hatimae akalipua gari hilo kwa kuligonga basi la wanajeshi wa Marekani lililolipuka na kupinduka, huku gari zote zilizokuwa karibu ya eneo hilo zikalipuka. Helikopta za NATO ziliwasili haraka katika eneo hilo kusafirisha majeruhi hospitalini.

Tukio hilo bila shaka katika kitongojii cha mji wa Kaboul ni ishara kwamba wapiganiaji wa Taliban hawana tena uwezo wa kushambuliia mjini kati kwa sasa baada ya ulinzi mkali kuzidishwa siku za nyuma kutokana na mashambulizi makubwa yaliotokea.

Asubuhi hii pia kusini mwa nchi hiyo askari wawili wa NATO kutoka Australia waliuawa na mtu alievalia sare za jeshi la Afghanistani ambae naye pia aliuawawa baadae. Mwanamke mmoja alijilipua pia mashariki mwa nchi hiyo katika ofisi za idara ya ujasusi bila hata hivyo kusababisha hasara yoyote.
 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.