Pata taarifa kuu
NEW ZELAND

Nahodha wa meli ya mizigo iliyovujisha mafuta New Zealand kufunguliwa mashtaka.

Nahodha wa meli ya mizigo iliyovujisha mafuta baharini nchini New Zealand amekamatwa na kushtakiwa kwa kusafirisha mizigo kinyume na taratibu jambo lililosababisha janga kubwa la mazingira ambalo lingeweza kuepukika.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Maafisa nchini humo wamethibitisha kushtakiwa kwa nahodha huyo ambaye taarifa zake za msingi zimehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ili kupisha uchunguzi na sheria kuchukua mkondo wake dhidi yake.

Maafisa wamesema kuvuja kwa mafuta baharini kumesababisha janga la mazingira katika nchini hiyo ambalo halijawahi kutokea,ambapo kikosi cha wanamaji kinachoshughulikia dharura nchini humo kimesema meli hiyo ilipakia makontena 11 yenye vifaa vya hatari ambavyo huweza kuwaka moto pindi vikigusana na maji.

Naye waziri wa mazingira Nick Smith amesema hilo ni janga la taifa hasa katika mazingira ya nchi hiyo ambapo mpaka sasa zaidi ya tani 350 za mafuta zinakadiriwa kuvujia baharini nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.