Pata taarifa kuu

Waziri wa ulinzi: India 'ina uwezo wa kuua' adui nchini Pakistan

Je, India ilifadhili mauaji yaliyolengwa nchini Pakistan? Akihojiwa na waandishi wa habari kufuatia kuchapishwa kwa uchunguzi wa gazeti la Guardian, Waziri wa Ulinzi wa India alieleza kuwa alikuwa akiwafuatilia magaidi, wakiwemo nje ya India. Katika miezi ya hivi karibuni, Canada na Marekani zimeshutumu India kwa kufanya mauaji katika ardhi yao.

Askari wa jeshi la India wakipiga doria kwenye mstari wa kusitisha mapigano kati ya India na Pakistani (picha ya kielelezo).
Askari wa jeshi la India wakipiga doria kwenye mstari wa kusitisha mapigano kati ya India na Pakistani (picha ya kielelezo). REUTERS/Mukesh Gupta/Files
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu huko Bangalore, Côme Bastin

Angalau mauaji ya watu ishirini nchini Pakistan yanahusishwa na idara ya ujasusi ya India, Gazeti la Guardian limedai wiki hii, likinukuu vyanzo visivyojulikana, vinavyoaminika nchini Pakistan na India. Bila kuthibitisha idadi ya watu waliouawa, Waziri wa Ulinzi Rajnath Singh hakukana habari hii.

"Tutaenda huko na kumuua"

"Iwapo gaidi yeyote wa Pakistani atajaribu kuvuruga usalama wa India au kufanya vitendo vya kigaidi katika ardhi yake," "tutajibu ipasavyo", amesema. Na hata akikimbilia Pakistan, tutaenda huko na kumuua. India sasa ina uwezo wa kufanya hivi, na Pakistan pia inaanza kutambua hilo. Sisi si wachokozi, tunataka uhusiano mwema na majirani zetu, lakini yeyote atakayetupa changamoto hataachwa. "

Jibu la wazi linapata msisimko fulani kwa kuzingatia mivutano ya sasa ya kidiplomasia kati ya New Delhi, Toronto na Washington. Mnamo Septemba 2023, Canada ilishutumu India kwa kupanga mauaji ya mwanaharakati Sikh karibu na Vancouver, anaetetea maeneo yao kujitawala. Muda mfupi baadaye, Marekani ilidai kuwa ilizuia mpango wa mauaji kwenye ardhi yake unaohusishwa na idara ya ujasiri ya India.

New Delhi yaakanusha

India inawachukulia Sikh, watu wanaotaka kujitenga - ambao wanadai serikali tofauti nchini India - kama magaidi. Hata hivyo, New Delhi, inakanusha kuandaa mauaji yaliyolengwa katika nchi ya kigeni. Wiki hii, idara ya ujasusi ya Canada pia ilishutumu India kwa kuingilia uchaguzi wake, ili kukabiliana na Sikh, wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya  wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa eneo lao wa Sikh. India pia inakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.