Pata taarifa kuu

Burma: Mabomu ya ardhini yalisababisha waathiriwa mara tatu zaidi katika mwaka 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limerekodi waathiririwa 1,052 -- watu 188 waliuawa na 864 kujeruhiwa -- mwaka 2023, ikilinganishwa na 390 mwaka uliopita. Kulikuwa na matukio 226 yaliyohusisha watoto, na kusababisha vifo vya watoto 59.

Mwanajeshi wa Burma (Myanmar) aliyejeruhiwa ambaye anajisalimisha kwa Kikosi cha Ulinzi cha Raia wa Karenni huko Loikaw, Myanmar, katika picha hii iliyopigwa mnamo Novemba 15, 2023.
Mwanajeshi wa Burma (Myanmar) aliyejeruhiwa ambaye anajisalimisha kwa Kikosi cha Ulinzi cha Raia wa Karenni huko Loikaw, Myanmar, katika picha hii iliyopigwa mnamo Novemba 15, 2023. via REUTERS - Karenni Nationalities Defense Fo
Matangazo ya kibiashara

Takriban 35% ya waathiriwa wanatoka eneo la Sagaing (kaskazini), ambalo lilikuja kuwa moja ya ngome za upinzani dhidi ya majenerali waaoshikilia madaraka baada ya mapinduzi ya 2021. Nchi imeharibiwa na mzozo wa wenyewe kwa wenyewe kati ya utawala na wapinzani wake wa kikabila na kisiasa.

Burma haijatia saini mkataba wa Umoja wa Mataifa unaopiga marufuku uzalishaji, uhifadhi na matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini.

Jeshi la Burma linashutumiwa mara kwa mara kwa kufanya ukatili na uhalifu wa kivita. Zaidi ya watu 6,000 wameuawa na wapiganaji wanaopinga mapinduzi na makundi ya makabila ya walio wachache, kulingana na utawala wa kijeshi. Ukandamizaji wa kijeshi dhidi ya aina zote za upinzani umesababisha vifo vya watu zaidi ya 4,800, kulingana nashirika la ndani la ufuatiliaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.