Pata taarifa kuu

Japani: Watu saba watafutwa baada ya kuanguka kwa ndege ya kijeshi ya Marekani baharini

Zoezi la utafutaji linaendelea Alhamisi kujaribu kupata watu saba waliotoweka baada ya ajali ya ndege ya jeshi la Marekani iliyotokea kwenye bahari ya Osprey siku moja kabla kusini magharibi mwa Japani, ambayo iliua mtu mmoja.

Osprey, nusu-ndege, nusu helikopta
Osprey, nusu-ndege, nusu helikopta AP - Darren England
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa wafanyakazi wa chombo hiki cha usafiri cha nusu-ndege, nusu helikopta alipatikana baharini akiwa amepoteza fahamu na akiwa katika mahutihuti siku ya Jumatano, na kifo chake kilithibitishwa baada ya kuhamishiwa katika hospitali ya Japan.

Kamandi Maalum ya Jeshi la Wanahewa la Marekani imesema Osprey CV-22B ilikuwa imebeba wafanyakazi wanane na "ilikuwa ikifanya mazoezi ya kawaida" kutoka Kambi ya Anga ya Marekani ya Yokota karibu na Tokyo.

"Chanzo cha ajali hiyo kwa sasa hakijajulikana," Kamandi Maalum ya Jeshi la Wanahewa la Marekani ilisema katika taarifa yake Jumatano, ikiongeza kuwa wafanyakazi wa dharura "wapo kwenye eeo la tukio na wanafanya shughuli za utafutaji na uokoaji."

Japani imewataka wanajeshi wa Marekani kusitisha safari za ndege zao za Osprey kwenye ardhi ya Japan hadi usalama wao "uimarishwe", isipokuwa ndege za aina hii zinazoshiriki katika "operesheni za utafutaji na uokoaji", Waziri wa Ulinzi wa Japani Minoru Kihara amesema Alhamisi.

Tokyo pia inaomba "kufichuliwa haraka kwa habari kuhusu mazingira ya ajali", ameongeza Bw. Kihara.

Jeshi la Japan tayari limesitisha safari za ndege zake za Osprey, amesema msemaji wa serikali ya Japan Hirokazu Matsuno, wakati akitoa salamu zake za rambirambi kwa wahanga waliofariki katika ajali hiyo.

- "Ndege na meli zimetumwa" -

Afisa wa usimamizi wa dharura katika idara ya Japan ya Kagoshima (kusini-magharibi), karibu na pwani ambayo ndege ilianguka, aliliambia shirika la habari la AFP Jumatano kwamba polisi wa eneo hilo walipokea "ripoti kwamba Osprey ilikuwa ikitema moto kutoka kwa injini yake ya kushoto" na ilipoteza sana mwinuko karibu na kisiwa cha Yakushima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.