Pata taarifa kuu

Australia yatoa hifadhi ya hali ya hewa kwa wakazi wa visiwa vya Tuvalu

Australia itawapokea wakimbizi wa hali ya hewa kutoka Visiwa vya Tuvalu. Ijumaa hii, Novemba 10, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ametangaza kuwa nchi hizo mbili zimetia saini makubaliano ya kuwaruhusu wakaazi 11,200 wa visiwa hivyo kuja na kuishi nchini Australia. Visiwa hivyo vinachukuliwa kuwa nchi ya kwanza ambayo kuwepo kwake kunatishiwa na ongezeko la joto duniani na kuongezeka kwa kina cha bahari.

Waziri wa Tuvalu akihutubia umaa huku miguu yake ikiwa ndani ya maji.
Waziri wa Tuvalu akihutubia umaa huku miguu yake ikiwa ndani ya maji. via REUTERS - Tuvalu Foreign Ministry
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Sydney, Léo Roussel

Hii ni hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa ambayo imetangazwa leo Ijumaa, Novemba 10 na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese. Akisafiri kwenda Visiwa vya Cook kwenye hafla ya Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki, ametangaza kutiwa saini kwa makubaliano na Tuvalu, ili kutoa uwezekano kwa wakaazi 11,200 wa visiwa hivyo, ambao wanazidi kutishiwa na kuongezeka kwa maji, kuishi Australia. Visa mpya itaundwa mahususi ili kuwahudumia wakimbizi hao wa hali ya hewa.

"Njia maalum"

“Australia itaweka mfumo hususan wa kuandikishwa ambao unaweza kuchukua hadi watu 280 kwa mwaka, njia ya pekee ya kuhama ili kuwezesha watu kutoka Tuvalu kuja Australia kuishi, kufanya kazi na kujifunza. " Visiwa viwili kati ya tisa vya Tuvalu tayari vimezama kwa kiasi kikubwa na wataalamu wanakadiria kwamba visiwa hivyo haviwezi kukaliwa kabisa ndani ya kipindi cha miaka 80.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.