Pata taarifa kuu

Japani: Afisa wa tatu wa serikali ya Kishida ajiuzulu

Nchini Japan, Waziri wa Mambo ya Ndani amejiuzulu kufuatia kashfa ya kifedha. Ni mjumbe wa tatu wa serikali kuondoka madarakani katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja na hivyo kudhoofisha nafasi ya Waziri Mkuu Fumio Kishida.

Vyombo vya habari vya Japan vinashangaa ni kwa muda gani Waziri Mkuu Fumio Kishida (picha yetu), aliye madarakani tangu 2021, ataendelea kushikilia wadhifa wake.
Vyombo vya habari vya Japan vinashangaa ni kwa muda gani Waziri Mkuu Fumio Kishida (picha yetu), aliye madarakani tangu 2021, ataendelea kushikilia wadhifa wake. AP - Toru Hanai
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe watatu wa taifa la tatu kwa uchumi duniani wamejiuzulu chini ya kipindi cha mwezi mmoja. Kutokana na msururu huu wa kujiuzulu, vyombo vya habari vya Japan vinajiuliza ni muda gani Waziri Mkuu Fumio Kishida, aliye madarakani tangu 2021, ataweza kuendelea kushikilia wadhifa wake. Anashikili mti ulio kauka kwenye kura za maoni. Umaarufu wake haukufikia 30%. Chini ya kizingiti hiki, siku zake za kisiasa zinahesabiwa.

Akabiliwa na mashtaka

Waziri wa Mambo ya Ndani Minoru Terada alikiri kwamba moja ya makundi yake yanayomuunga mkono yalikuwa yamewasilisha ripoti iliyotiwa saini ya ufadhili wa kisiasa kutoka kwa mtu aliyefariki. Mashtaka mengine yanahusiana na malipo haramu wakati wa kampeni zake za kuchaguliwa tena katika Baraza la wawakilishi.

Wajapani hawajamsamehe Waziri Mkuu, Fumio Kishida, kwa kuandaa, bila mashauriano na kwa gharama kubwa, mazishi ya serikali ya mkuu wa zamani wa serikali Shinzo Abe aliyeuawa mwaka huu. 

Uhusiano na dhehebu ya Mwezi

Kufuatia kuuawa kwake, vyombo vya habari vilifichua uhusiano wa kindugu uliodumishwa, kwa miongo kadhaa, na chama cha kihafidhina - kilicho na viti vingi bungeni - na dhehebu la Mwezi (linaojulikana kwa jina la Kanisa la muungano huko Japani). Nusu ya wabunge wa Conservative wanadai kuwa ni waumuni wa kanisa hilo, hasa wakati wa kipindi cha uchaguzi. Kundi hilo la kidini linashukiwa kuwahadaa wafuasi wake na kuwaharibu baadhi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.