Pata taarifa kuu

Ukraine: Zelensky, Erdogan na Guterres kukutana Alhamisi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan watakutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Alhamisi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atakuwa na mazungumzo na marais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, siku ya Alhamisi, Agosti 18, 2022.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atakuwa na mazungumzo na marais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, siku ya Alhamisi, Agosti 18, 2022. AP - Yuki Iwamura
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atasafiri kuelekea Ukraine siku ya Alhamisi ambapo atashiriki katika mkutano na Marais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, msemaji wake ametangaza Jumanne.

"Kwa mwaliko wa Rais Volodymyr Zelensky, Katibu Mkuu atakuwa Lviv siku ya Alhamisi kushiriki katika mkutano wa pande tatu na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kiongozi wa Ukraine," Stéphane Dujarric amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akibainisha kuwa Antonio Guterres kisha atasafiri hadi Odessa siku ya Ijumaa, kisha Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.