Pata taarifa kuu

Kesi ya kadinali anayeunga mkono demokrasia yatatiza uhusiano wa Vatican na Beijing

Wanachama sita wa mfuko wa misaada ya pande zote kwa wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wamefikishwa mahakamani huko West Kowloon Jumanne hii asubuhi. Miongoni mwao ni Margaret Ng, mwanasheria maarufu wa haki za binadamu na Denise Ho, mwigizaji wa nyimbo za canto-pop, na Kadinali Zen mwenye umri wa miaka 90.

Kardinali Chen Rijun, askofu mstaafu wa dayosisi ya Hong Kong, alikamatwa na polisi Mei 3 kwa tuhuma za kukiuka sheria ya usalama wa taifa.
Kardinali Chen Rijun, askofu mstaafu wa dayosisi ya Hong Kong, alikamatwa na polisi Mei 3 kwa tuhuma za kukiuka sheria ya usalama wa taifa. © 图取自facebook.com/cardzen
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii ya kiongozi wa kanisa la chinichini la China inaiweka Vatican katika uhusiano mgumu na Beijing.

Washtakiwa sita waliofika Jumanne asubuhi wote walikana mashtaka: Wanashtakiwa kwa kutosajili ipasavyo hazina ya misaada ya pande zote, "6.12", ambayo walikuwa wameianzisha kusaidia wanaharakati waliokamatwa na polisi wakati wote wa maandamano ya mwaka 2019 Tarehe ya kesi imepangwa Septemba 19.

Mashitaka haya hayaeleweki na haya msingi- na upande wa utetezi unakusudia kuonyesha kwamba mfuko huu haukufanya makosa ya kiutawala. Lakini mashitaka haya ya watu mashuhuri na wanaoheshimika wa mashirika ya kiraia, miongoni mwa waliosalia kwa jumla huko Hong Kong, yanaonyesha jinsi mamlaka ilivyo tayari kwenda kutisha wanaharakatiwananaotetea haki za wanyonge.

"Kadinali Zen daima amekuwa sauti yenye nguvu na kumbukumbu ya maadili sio tu kwa Wakatoliki na Wakristo lakini kwa watu wa asili zote na imani zote", kasisi wa Argentina, Gervais Baudry, amekumbusha nje ya mahakama. "Kwa hivyo watu wengi leo wana wasiwasi juu ya kile kinachotokea dhidi yake"

Mbali na viongozi kadhaa wa kidini, wanadiplomasia kumi na wawili walikwenda katika mahakama ya West Kowloon asubuhi ya leo na kuonyesha kwamba, kati ya kesi nyingi zinazoendelea hivi sasa huko Hong Kong dhidi ya wanaharakati wanaounga mkono demokrasia, hii ni ya kipekee.

Kukamatwa kwa Joseph Zen mapema mwezi wa Mei chini ya sheria ya usalama wa taifa kulishtua jamii ya Wakatoliki katika jiji hilo. Inaleta hofu ya kuongezeka kwa visa vya uchunguzi dhidi ya dini zote, katika jiji ambalo wanaharakati wengi wa demokrasia ni Wakristo.

Pia inakuja wakati mgumu kwa Bunge la Holy See, ambalo linajadiliana kuhusu kurejeshwa kwa makubaliano yenye utata na Beijing juu ya uteuzi wa maaskofu, suala la mzozo kati ya Kanisa Katoliki na serikali ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.