Pata taarifa kuu
BURMA-USALAMA

Burma: Urusi, China na Serbia zaendelea kutoa silaha kwa utawala wa kijeshi

Urusi, China na Serbia zimeendelea kuwapa silaha utaalawa kijeshi wa Burma, Umoja wa Mataifa unashutumu, huku raia zaidi ya 1,500 wameuawa tangu mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, 2021.

Tangu Februari 2021, zaidi ya raia 1,500 wameuawa na laki kadhaa wamelazimika kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa,
Tangu Februari 2021, zaidi ya raia 1,500 wameuawa na laki kadhaa wamelazimika kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa, REUTERS - Stringer .
Matangazo ya kibiashara

Urusi, China na Serbia zimeendelea kusambaza silaha kwa utawala wa kijeshi la Burma, ambazo zimetumika kushambulia raia tangu mapinduzi, ripota maalum wa Umoja wa Mataifa Tom Andrews alisema Jumanne. Ripota huyu maalum wa Umoja wa Mataifa alitoa wito wa kuitishwa kwa dharura kwa kikao cha Baraza la Usalama a Umija wa Mataifa ili "kupitisha azimio ambalo kwa uchache linakataza uhamishaji wa silaha huu ambao jeshi la Burma hutumia kushambulia na kuua raia", kulingana na taarifa.

"Licha ya ushahidi wa ukatili uliofanywa na utawala wa kijeshi bila kuadhibiwa tangu mapinduzi ya mwaka jana, Urusi na China, wanachama wa Baraza la Usalama wameendelea kusambaza utawala wa kijeshi wa Burma wapiganaji wengi na magari ya kivita," amebaini Tom Andrews. "Serbia iliidhinisha usafirishaji wa roketi na silaha kwa jeshi la Burma".

Ametaja hasa ndege za kivita za JF-17 au hata makombora, roketi, makombora na risasi nyinginezo. Kwa ripota maalum, hakuna hata nchi moja kati ya ya nchi zilizowasilisha silaha "hazingeweza kufahamu au angalau kushuku" kwamba angalau tangu 2018 silaha zilizouzwa kwa Burma zingetumika katika mashambulizi dhidi ya raia kinyume na sheria za kimataifa.

Tangu Februari 2021, zaidi ya raia 1,500 wameuawa na laki kadhaa wamelazimika kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa, huku serikali ikikandamiza vikali harakati za maandamano. Umoja wa Mataifa unachunguza uhalifu dhidi ya binadamu unaoweza kuwa ulitokea baada ya ripoti za mauaji ya wanavijiji na mamia ya nyumba kuteketezwa.

Kwa kuwa China na Urusi ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama na hivyo wana haki ya kupiga kura ya turufu, azimio la vikwazo vya kiuchumi haliwezi kufanikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.