Pata taarifa kuu
EU-USHIRIKIANO

Umoja wa Ulaya wataka kujenga tena uaminifu na Marekani

Mazungumzo yaliyosubiriwa kwa muda mrefu kati ya Emmanuel Macron na Joe Biden yamewezesha taarifa ya pamoja ya maridhiano. Wiki moja baada ya kutangazwa kwa ushirikiano wa nchi tatu, AUKUS, kati ya Australia, Uingereza na Marekani, marais wa Ufaransa na Marekani wameanza tena mazungumzo na matokeo yake ni mazuri kwa ushirikiano ulioimarishwa.

Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Maswala ya Kigeni na Sera ya Usalama Josep Borell akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kando ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa Septemba 22, 2021 huko New York.
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Maswala ya Kigeni na Sera ya Usalama Josep Borell akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kando ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa Septemba 22, 2021 huko New York. AFP - JASON DECROW
Matangazo ya kibiashara

Ushirikiano huu lazima pia uhusu Muungano wa Ulaya, uliotajwa mara kadhaa katika tangazo la pamoja, kulingana na mkuu wa sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.

 

Baada ya mazungumzo kati ya marais wa Ufaransa na Marekani, Josep Borrell amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Mkutano huo ulikuwa fursa kwa mkuu wa sera za Mambo ya Nje wa Ulaya kusisitiza ukweli na kutuma ujumbe sawa na ule wa Ufaransa. "Lazima tufanye kazi ili kujenga tena imani ya ukanda wa transatlantic," amesema Josep Borrell, baada ya taarifa za marais hao wawili.

Kulingana na marais hao wawili, ushiriki wa Ufaransa na Umoja wa Ulaya katika eneo la Indo-Pacific ni muhimu sana.

Maslahi ya EU: kuwekeza katika Indo-Pacific

Kwa EU, kwa hivyo, kuna sababu mbili za kutumia taarifa hii. Kwanza, kwa sababu Umoja wa Ulaya umeamua kushikamana na Ufaransa: baada ya siku chache za mvutano, sasa wanakiri kuwa ukanda wa transatlantic kwa ujumla umedhoofika. Pili, kwa sababu maslahi ya Umoja wa Ulaya ni kuwekeza katika eneo hili. Eneo ambalo limekuwa kituo kipya cha mvuto wa dunia, kulingana na Josep Borrell.

Ushirikiano wa pande tatu ulitangazwa ssiku mja baada ya kuwasilishwa kwa kakati wa Ulaya kwa ukanda wa Indo-Pacific. Umoja wa Ulaya sasa unatarajia kuhusishwa na mipango ya Marekani katika eneo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.