Pata taarifa kuu
UFILIPINO-SIASA

Bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao ajitangaza mgombea urais 2022

Bondia Manny Pacquiao ametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa 2022 nchini Ufilipino, na kumaliza miezi kdhaa ya uvumi kuhusiana na kuwania kwake katika uchuguzi huo.

Manny Pacquiao, Januari 24, 2019 huko Manila.
Manny Pacquiao, Januari 24, 2019 huko Manila. Ted ALJIBE AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wakati umewadia, tuko tayari kushiriki katikakinyang'anyiro cha urais," amesema nyota huyo wa ndondi nchini Ufilipino, 42, ambaye amekubali kupeperusha bendera ya tawi lililojitenga na chama cha rais Rodrigo Duterte.

Bondia huyo alifanya uamuzi wake wiki chache baada ya pambano lake la mwisho la ndondi dhidi ya raia wa Cuba, Yuben Yordenis Ugas, ambapo alishindwa Agosti 22 huko Las Vegas.

Bondia pekee aliyewahi kuwa bingwa wa ulimwengu katika daraja nane tofauti za uzani, "Pac Man" ni sifa kubwa kwa Wafilipino.

Alipokuwa mtoto, aliishi mitaani kabla ya kuingia kwenye ndondi za Januari 1995 kwa fedha za peso 1,000 (sawa na euro 19) na baadaye akajilimbikizia utajiri unaokadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni 500.

Manny Pacquiao aliingia katika siasa mnamo 2010, wakati alipochaguliwa kuwa mbunge, kabla ya kuwa seneta mnamo 2016. Wakati mwingine alizua sintofahamu kwa kauli zake kwa kuunga mkono adhabu ya kifo au kupinga ushoga.

Lakini yeye ni maarufu sana katika visiwa hivyo, ambapo ukarimu wake na njia yake ya kufanikiwa wakati alizaliwa katika umasikini uliokithiri hupendekezwa sana.

Pacquiao tayari ameahidi kutofanya juhudi yoyote, akianza kwa kutuma "mamia au maelfu" ya wanasiasa wapotovu kwenye "gereza kubwa" lililojengwa.

"Kwa wale wote wanaoniuliza ni ustadi gani na uwezo gani, je! Umewahi kupata njaa?" Alisema Jumapili mbele ya wafuasi wake. "Je! Unajua ni nini kukosa chakula, kukopa pesa kutoka kwa majirani zako au kungojea mabaki ya chakula yaliyokusanywa kwenye migahawa? Manny Pacquiao aliye mbele yenu hapa alipitia mazingira hayo na kwani alizaliwa katika familia masikini".

Hadi hivi majuzi, Pacquiao alikuwa msaidizi mashuhuri wa rais Duterte na vita vyake vyenye utata juu ya dawa za kulevya, ambazo waendesha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wanataka kuchunguza kwa madai ya mauaji yasiyokuwa halali ya makumi ya maelfu ya watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.