Pata taarifa kuu
INDIA-AFYA

Zaidi ya vifo 4,000 na kesi mpya 400,000 za maambukizi zaripotiwa India

India imerekodi leo Jumamosi idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na COVID-19 kwa siku moja na watu 4,187 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo, na kusababisha idadi ya vifo kufikia karibu 240,000 nchini humo.

Wahudumu wa afya wakibeba mwili wa mtu aliyefariki kutokana na COVID-19, katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Ahmedabad, India, Mei 8, 2021.
Wahudumu wa afya wakibeba mwili wa mtu aliyefariki kutokana na COVID-19, katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Ahmedabad, India, Mei 8, 2021. REUTERS - AMIT DAVE
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya visa vipya vya maambukizi vilivyogunduliwa katika muda wa saa 24 ni zaidi ya 400,000 kwa siku ya tatu mfululizo (401,078) kwa jumla ya watu milioni 21.9 walioambukizwa.

Wakati huo huo majimbo mawili ya kusini mwa India yamewekewa masharti ya kutotoka nje, wakati visa vya maambukizi ya Corona vikipanda maradufu, huku serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi ikiendelea kupata shinikizo la kuweka vizuizi vya kitaifa kukabiliana na janga la Corona. 

Mji ulioathirika zaidi ni Bengaluru katika jimbo la Karnataka ulio na zaidi ya watu laki tatu walioambukizwa. Lakini wataalamu wanasema hali huenda ikazidi kuwa mbaya kufuatia mji wa tatu kwa ukubwa nchini India, kukumbwa na uhaba wa gesi ya Oksijeni, hospitali zilizojaa watu na kujaa pia kwa maeneo ya kuchomea maiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.