Pata taarifa kuu
G7-INDIA-AFYA

Hofu yatanda G7 baada ya baadhi wajumbe kutoka India kupatikana na maambukizi

Ujumbe mzima wa India unaoshiriki katika mkutano wa kundi la mataifa tajiri, G7,  huko London umewekwa karantini baada ya wajumbe wawili kupatikana na maabukizi ya COVID-19, serikali ya Uingereza imetangaza leo Jumatano.

Wawakilishi kutoka mataifa ya G7 wanashiriki katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 huko London, Uingereza, Mei 5, 2021.
Wawakilishi kutoka mataifa ya G7 wanashiriki katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 huko London, Uingereza, Mei 5, 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

"Watu wawili kutoka ujumbe wa India wamepimwa na kupatikana na maabukizi ya virusi vya Corona, kwa hivyo ujumbe wote sasa umewekwa karantini," afisa wa Uingereza amesema.

"Mkutano wa G7 umeweza kufanyika kutokana na itifaki kali ya afya, pamoja na uchunguzi wa kila siku wa wajumbe wote," ameongeza.

Waziri wa Mambo ya nje wa India Subrahmanyam Jaishankar hakupatikana na virusi vya Corona, ameaandika mwandishi wa kituo cha Sky News Joe Pike kwenye akaunti yake ya Twitter. Waziri wa India alikutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Priti Patel siku ya Jumanne.

Subrahmanyam Jaishankar amesema Jumatano atashiriki vikao vya G7 vinavyoendelea London.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.