Pata taarifa kuu
G7-MAREKANI

Coronavirus: Biden kukutana na viongozi wa G7 Ijumaa

Rais wa Marekani Joe Biden atakuwa mwenyeji wa hafla yake ya kwanza na viongozi wa kundi la nchi 7 zenye uchumi wa juu (G7) Ijumaa - kujadili kuhusu janga la Corona na uchumi wa dunia - Ikulu ya White House imebaini.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Kwa Joe Biden hii itakuwa "fursa ya kujadili mipango ya kushinda janga la COVID-19 na kujenga upya uchumi wa dunia," White House imeongeza katika taarifa.

Hivi karibuni rais wa Marekani Joe Biden alikosoa mpango wa chanjo wa mtangulizi wake Donald Trump na kuwataka Wamarekani kuwa wavumilivu wakati akiendelea kurekebisha mapungufu katika vita dhidi ya janga la Corona.

Joe Biden alisema Donald Trump, ambaye alitumia zaidi ya miezi yake miwili kujaribu - bila mafanikio - kubadili matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba, hakuagiza chanjo za kutosha au kuchukuwa hatua za kutosha ili raia waweze kupewa chanjo.

Marekani ni nchi ya kwanza duniani kuathirika zaidi na ugonjwa huo kwa visa vya maambukizi na vifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.