Pata taarifa kuu
IRAN

Khamenei alaani matamshi ya Javad Zarif dhidi ya Soleimani

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amelaani matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na kusema kuwa ni "kosa kubwa" baada ya kuvuja kwa rekodi ambayo Mohammad Javad Zarif anaonekana kukosoa ushawishi wa jeshi katika masuala ya diplomasia.

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei. - KHAMENEI.IR/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Sera ya nchi inashughulikia masuala ya kiuchumi, kijeshi, kijamii, kisayansi na kiutamaduni, pamoja na uhusiano wa nje na diplomasia," Ali Khamenei amebaini katika hotuba ya televisheni.

Kama "mmoja anamkana mwengine au anapingana na mwingine, inakuwa haina maana. Hakuna kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu anayepaswa kufanya kosa kubwa kama hilo, ”akaongeza.

Wakati huo huo Waziri Mohammad Javad Zarif ameomba "msamaha" kwa familia ya Soleimani kwa matamshi yake.

"Natumai familia inayoheshimiwa ya Jenerali Qassem Soleimani itanisamehe," waziri huyo ameandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Tangu kuchapishwa kwa rekodi hii na vyombo vya habari vya Iran vilio nje ya nchi, wahafidhina wameendelea kumkosoa waziri wa mambo ya nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.