Pata taarifa kuu
UTURUKI

Watu 532 wenye uhusiano na Gülen wasakwa na Uturuki

Uturuki imeagiza kukamatwa kwa watu 532, ikiwa ni pamoja na watu 459 kutoka upande wa jeshi, kutokana na uhusiano wao na mhubiri aliyekimbilia uhamishoni nchini Marekani Fethullah Gülen, shirika la habari la Anadolu limeripoti leo Jumatatu.

Mhubiri wa Uturuki Fethullah Gülen, ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Marekani, hapa ilikuwa Julai 10, 2017 nyumbani kwake huko Pennsylvania.
Mhubiri wa Uturuki Fethullah Gülen, ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Marekani, hapa ilikuwa Julai 10, 2017 nyumbani kwake huko Pennsylvania. REUTERS/Charles Mostoller
Matangazo ya kibiashara

Fethullah Gülen, ambaye anaishi uhamishoni nchini Marekani, anatuhumiwa na Uturuki kwa kupanga mapinduzi yaliyoshindwa ya mwezi Julai 2016 dhidi ya Rais Recep Tayyip Erdogan. Mhubiri huyo ameendelea kukanusha madai hayo.

Shirika la habari la Anadolu limeripoti kuwa operesheni iliyofanywa katika jumla ya majimbo 62, kwa ombi la waendesha mashtaka, limewezesha kukamatwa kwa washukiwa 258, wakiwemo maafisa wanne wa jeshi wenye vyeo vya kanali, luteni kanali, makamanda tisa na manahodha 24.

Wanajeshi wengi wahusishwa katika jaribio la mapinduzi

Ofisi ya mwendesha mashtaka ya Izmir (magharibi mwa Uturuki) kwa upande wake imeomba kukamatwa kwa watu 274, wengi wao wakiwa ni wanajeshi, shirika la habari la Andalou limeogeza.

Tangu jaribio la mapinduzi la mwezi Julai 2016, karibu watu 80,000 wamekamatwa na wanasubiri hukumu wakati maafisa 150,000 wa serikali wamefukuzwa kazi au kusimamishwa kazi. Zaidi ya wanajeshi 20,000 wamefukuzwa kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.