Pata taarifa kuu
UTURUKI-SIASA-USALAMA

Uturuki yatoa Waranti wa kukamatwa dhidi ya wafuasi 304 wa Gülen

Uturuki imeagiza kukamatwa kwa wanajeshi 304 katika operesheni inayolenga watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa mhubiri Fethullah Gülen, ambaye anatuhumiwa kupanga mapinduzi yaliyotibuliwa mwaka 2016, limeripoti shirika la habari la serikali la Anatolia.

Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki
Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki Presidential Press Office/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangu jaribio la mapinduzi la Julai 2016, ambapo Gülen - anayeishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1999 - anaendelea kukanusha kuhusika kwake, watu 80,000 wamewekwa kizuizini na karibu maafisa 150,000 wamefukuzwa au kusimamishwa kazi katika sekta ya elimu, jeshi na sekta zingine.

Operesheni ya Jumanne imezinduliwa na ofisi ya mashtaka katika mkoa wa pwani wa Izmir, magharibi mwa Uturuki, na inawalenga washukiwa kutoka zaidi ya mikoa 50, shirika la Anatolia limesema.

Wapinzani wa rais Recep Tayyip Erdogan wanamtuhumu rais huyo kwa kutumia jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwaka 2016 kama kisingizio cha kukandamiza mtu yeyote anayethubutu kufungua mdomo kwa kukosoa utawala wake.

Serikali imekanusha madai hayo na kubaini maswala ya usalama wa kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.