Indonesia yapata sehemu ya mabaki ya manowari iliyotoweka
Timu za Indponesia zinazoshiriki katika shughuli ya utaftaji wa manowari iliyotoweka zmefanikiwa kupata sehemu ya mabaki yanayoshukiwa kuwa ya manowari hiyo iliyotoweka katika Bahari ya Bali Jumatano wiki , amesema mkuu wa kikosi cha jeshi la wanamaji nchini Indonesia.
Imechapishwa:
Awali jeshi la Wanamaji la Indonesia limesema limetuma helikopta na meli maalum katika shughuli ya utaftaji katika eneo ambalo manowari ya KRI Nanggala-402 ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano, ilipokuwa ikijiandaa kwa mazoezi ya kijeshi
Mamlaka nchini indonesia imebaini kwamba manowari hiyo imeonekana kwenye urefu wa mita 850 za kina, ikiwa ni chini sana kuliko kina chake cha juu cha kupiga mbizi, ambacho ni mita 500.
Marekani, Australia ana India wametuma vikosi vyao kusaidia kuipata manowari hiyo manowari hiyo iliyotoweka wakati wa mazoezi ya kijeshi.