Indonesia: Hakuna matumaini ya kuipata manowari iliyopotea
Marekani imepeleka ndege ya P-8 Poseidon kushiriki katika shughuli ya utaftaji na uokoaji wa manowari ya Jeshi la Wananchi la Indonesia iliyopotea katika Bahari ya Bali, huku kukiwa na matumaini madogo ya kupata wafanyakazi 53 wa manowari hiyo wakiwa hai.
Imechapishwa:
Jeshi la Wanamaji la Indonesia limesema limetuma helikopta na meli maalum katika shughuli ya utaftaji katika eneo ambalo manowari ya KRI Nanggala-402 ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano, ilipokuwa ikijiandaa kwa mazoezi ya kijeshi.
Australia pia imetumia meli kubwa iliyosheheni helikopta na vifa vingine vingi kusaidia katika shughuli ya utaftaji, wakati meli ya uokoaji kwenye maji ya kina iko njiani kutoka India, huku kukiwa na wasiwasi mkuwa juu ya uwezekano wa kwamba manowari ilizamishwa n kuharibiwa vibaya na nguvu kubwa ya maji.