Pata taarifa kuu
INDIA

Coronavirus: Rekodi ya kila siku ya visa vipya vya maambukizi yaripotiwa India

India imerekodi visa vipya 346,786 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika kipindi cha saa 24 zilizopita, kulingana na takwimu za serikali zilizotolewa leo Jumamosi, ikiwa ni rekodi mpya ya dunia katika nchi ambayo hospitali zinatoa wito wa kuongezwa kwa akiba ya oksijeni.

Wafanyakazi wa afya waliovaa vifaa vya kujikinga (PPE) wakibeba miili ya watu ambao walikuwa wanaugua ugonjwa wa corona (COVID-19), nje ya hospitali ya Guru Teg Bahadur, huko New Delhi, India, Aprili 24, 2021
Wafanyakazi wa afya waliovaa vifaa vya kujikinga (PPE) wakibeba miili ya watu ambao walikuwa wanaugua ugonjwa wa corona (COVID-19), nje ya hospitali ya Guru Teg Bahadur, huko New Delhi, India, Aprili 24, 2021 REUTERS - ADNAN ABIDI
Matangazo ya kibiashara

India inakumbwa na mlipuko wa pili wa janga kali ambalo huua mtu kila baada ya dakika nne huko Delhi, eneo ambapo mfumo wa hospitali unaofadhiliwa unashindwa kukidhi mahitaji ya huduma.

Serikali imepeleka ndege za kijeshi na treni kuleta oksijeni kutoka kote nchini hadi mji mkuu.

"Tafadhali tusaidie kupata oksijeni. Kuna hatariya kutokea maafa makubwa hapa," Waziri Mkuu wa serikali ya Delhi Arvind Kejriwal alimwambia Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika mkutano Ijumaa wiki hii.

Mgogoro huo pia unaripotiwa katika maeneo mengine ya nchi, ambapo hospitali kadhaa pia zimetangaza kwamba zimeishiwa na oksijeni kwa matumizi ya matibabu. Kulingana na vyombo vya habari vya India, watu kadhaa wamefariki dunia hivi majuzi katika miji ya Jaipur na Amritsar kwa sababu ya ukosefu wa gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.