Pata taarifa kuu
INDIA

Virusi: Visa vipya 315,000 vyaripotiwa india, rekodi ya dunia

India imetangaza leo Alhamisi karibu kesi mpya 315,000 za maambukizi ya virusi vya Corona katika kipindi cha saa 24, hii ikiwa ni rekodi ya dunia, wakati hospitali za New Delhi zinakabiliwa na uhaba wa oksijeni.

Visa vya maambukizi vyaendelea kuripotiwa kwa wingi nchini India.
Visa vya maambukizi vyaendelea kuripotiwa kwa wingi nchini India. NARINDER NANU AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko wa pili wa janga hili, ambao lumesababishwa hasa na "aina mbili za virusi" vya Corona na kuendelea kuwepo kwa mikusanyiko ya watu wengi vimesababisha maambukizi zaidi, na hivyo kuia mashakani mfumo wa afya nchini India.

Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 314,835 vya maambukizi, ripoti ya kila siku ambayo hakuna nchi yoyote duniani iliwahi kurekodi hapo awali. Pamoja na idadi hii mpya India sasa imefikisha idadi rasmi ya visa milioni 15.9 vya maambukizi,ikiwa ni nchi ya pili iliyoathirika zaidi na janga hilo duniani.

Jumla ya vifo 2,074 vimerekodiwa kwa kipindi cha zaidi ya saa 24 nchini India, na kufanya idadi vifo kufikia karibu 185,000. Idadi ya visa vya maambukizi na vifo kwa kila kata, hata hivyo, bado iko chini sana nchini India kuliko nchi nyingine nyingi.

Siku ya Jumapili Waziri Mkuu Narendra Modi alitoa wito kwa raia wake kukabilian vilivgo na janga la COVID-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.