Pata taarifa kuu
JAPANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Japani yapanga kuchukuwa hatua za dharura kwa miezi sita

Serikali ya Japani imepanga kutangaza hali ya dharura ya miezi sita kutokana na janga la Covid-19, kituo cha televisheni cha TBS kimeripoti leo Jumatatu.

Waziri Mkuu Shinzo Abe na Waziri wa Afya Katsunobu Kato katika mkutano wa dharura kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19, Tokyo Februari 14, 2020.
Waziri Mkuu Shinzo Abe na Waziri wa Afya Katsunobu Kato katika mkutano wa dharura kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19, Tokyo Februari 14, 2020. STR / JIJI PRESS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hizo zitahusu Tokyo na wilaya tatu jirani na mji mkuu, pamoja na jimbo la Osaka, TBS imeongeza. Katika kipindi hiki, wilaya hizo zingeamua muda wa utekelezaji wa hatua zao, kituo cha televisheni cha TBS kimeongeza.

Hali ya dharura inaweza kutangazwa kuanzia Jumanne, imebaini TBS.

Kulingana na gazeti la kila siku la Nikkei, baraza la ushauri juu ya janga hilo, lililoteuliwa na serikali, limekuwa likikutana tangu saa 05:00 Alfajiri (saa za kimataifa) kwa ajili ya mkutano wa maandalizi baada ya Waziri Mkuu, Shinzo Abe kutangaza hali ya dharura.

Serikali ya Japani iko chini ya shinikizo la kuchukua hatua hizi katika kukabiliana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Kulingana na ripoti ya hivi karibuni, zaidi ya visa 4 500 vya maambukizi vilivothibitishwa vimeripotiwa nchini Japani, pamoja na vifo vya watu 110.

Mageuzi ya sheria yaliyopitishwa mwezi uliopita kama sehemu ya majibu ya serikali kwa janga la SARS-CoV-2 yanamruhusu Waziri Mkuu kutangaza hali ya dharura ikiwa ugonjwa utasababisha "hatari kubwa" na ikiwa kusambaa kwa ugonjwa huo kunaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi.

Kutangazwa kwa hali ya dharura kutawaagiza wakuu wa mikoa kuwatolea wito raia kubaki nymbani na makampuni kufungwa, lakini kutotangaza marufuku ya jumla ya kubaki nyumbani kwa nchi nzima kama ilivyofanya Italia, Uhispania na Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.