Pata taarifa kuu
INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Rekodi mpya ya visa vya kila siku yathibitishwa India

India imerekodi visa vipya 78,266 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, ikiwa ni idadi kubwa tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na Wizara ya Afya ya India.

India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na janga hili baada ya Marekani na Brazil.
India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na janga hili baada ya Marekani na Brazil. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la Reuters linabaini kwamba takwimu rasmi inaonyesha kwamba hii pia ni rekodi ya kesi za kila siku zilizoripotiwa duniani kote tangu Agosti 7.

Kufikia sasa idadi ya visa vya maambukizi nchini kote China imefikia zaidi ya kesi milioni 3.39 na vifo 61,529, ikiwa ni pamoja na vifo vipya 1,057 vilivyorekodiwa katika muda saa ishirini na nne zilizopita.

India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na janga hili baada ya Marekani na Brazil.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.