Pata taarifa kuu
URUSI-SIASA-USALAMA

Dmitri Medvedev atangaza kujiuzulu kwa serikali ya Urusi

Waziri Mkuu wa Urusi amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa serikali yake kwa Rais Vladimir Putin Jumatano wiki hii. Taarifa hiyo ilikuja muda mfupi baada ya Rais Vladimir Putin kutoa hotuba yake ya mwaka kuhusu hali ya nchi.

Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev.
Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev. Sputnik/Dmitry Astakhov/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo ambalo limewashangaza wengi nchini Urusi, linakuja baada ya hotuba ya rais wa nchi hiyo Vladimir Putin kutangaza marekebisho ya katiba.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya Urusi, Dmitry Medvedev ameeleza kwamba "Sisi, kama serikali ya ya Urusi tunapaswa kumpa rais wa nchi yetu nafasi ya kuchukua hatua zote muhimu. Hii ndio sababu [...] serikali kwa ujumla imejiuzulu. "

Baada ya kukubali kujiuzulu kwa serikali hiyo kujiuzulu, Rais Putin amewataka mawaziri kufanya kazi kama serikali ya mpito hadi serikali mpya itakapoundwa.

Kabla ya kutangaza kujiuzulu kwa baraza la mawaziri, Medvedev alikutana na Putin kujadili hotuba yake kuhusu hali ya nchi, ambayo aliitoa mapema leo Jumatano, ofisi inayohusika na upashaji habari ya Kremlin imesema.

Putin pia amesema ana mpango wa kuweka wadhifa wa naibu katibu wa Baraza la Usalama la Urusi na kuumpendekezea Medvedev.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.