Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI- KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Korea Kaskazini: Jaribio la kurusha makombora ni "onyo" kwa Washington na Seoul

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema jaribio la kurusha makombora la hivi karibuni la Korea Kaskazini ni "onyo" kwa Washington na Seoul kwa sababu ya mazoezi yao ya pamoja la kijeshi , shirika la habari la serikali la KCNA limeripoti leo Jumatano.

Hivi karibuni Korea Kaskazini ilirusha makombora ya masafa marefu.
Hivi karibuni Korea Kaskazini ilirusha makombora ya masafa marefu. Korean Central News Agency (KCNA)
Matangazo ya kibiashara

Jaribio la makombora la hivi karibuni lilifanyika Jumanne baada ya vikosi vya Marekani na Korea Kusini siku moja baada ya kuzinduliwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini lenye lengo la kutathmini uwezo wa Seoul wa kuwa na udhibiti wa kazi wakati wa vita.

Pyongyang ilionya kwamba uzinduzi wa mazoezi hayo utahatarisha mazungumzo ambayo yanatarajiwa kuanza tena kati ya Marekani na Korea Kaskazini kuhusu silaha za nyuklia za Pyongyang.

Korea Kaskazini imekuwa ikilaani mazoezi hayo ya kijeshi ya pamoja ikiyachukuliwa kama maandalizi ya uvamizi wa ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.