Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI- KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Nyuklia: Korea Kaskazini yazua sintofahamu baada ya jaribio lake la makombora

Korea Kaskazini imetangaza leo Ijumaa kwamba jaribio lake la "makombora ya masafa marefu" limefana kwa kiasi kikubwa, kauli ambayo imeendelea kuzidisha mvutano na Marekani.

Picha iliyotolewa Mei 10, 2019 na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini Kcna la jaribio la kijeshi la makombora nchini Korea ya Kaskazini.
Picha iliyotolewa Mei 10, 2019 na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini Kcna la jaribio la kijeshi la makombora nchini Korea ya Kaskazini. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amesema ana imani kuwa hakuna mtu "amefurahishwa" na jaribio la makombora ya Korea Kaskazini.

Mkutano wa pili kati ya rais wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini Jong Un ulimalizika bila makubaliano yoyote mnamo mwezi Februari jijini Hanoi. Hata hivyo viongozi hao wawili hawakuweza kutoka taarifa ya pamoja kuhusu suala nyeti la nyuklia.

Wawili hawa hawakuweza kukubaliana juu ya masharti ya kuondoa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Korea Kaskazini na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini baada ya kuondolewa vikwazo hivyo.

Tangu wakati huo, kiongozi wa Korea Kaskazini ametilia mashaka nia njema ya Washington na kuomba Marekani kubadili mwenendo.

Siku ya Alhamisi, Korea Kaskazini "ilifanya jaribio la makombora mawili yanayoonekana kuwa ni ya masafa mafupi," Kamati ya wakuu wa majeshi nchini Korea Kusini imesema katika taarifa. Makombora hayo yaliyorushwa kutoka Mkoa wa Pyongan Kaskazini, yalisafiri kilomita 270 na 420 mashariki mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.