Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-UHASAMA-USALAMA

Hali ya taharuki kati ya Marekani na Iran yaendelea kuongezeka

Iran imeendelea kudai kuwa imewakamata majasusi 17 ambao inasema wamekuwa wakifanyia kazi shirika la ujasusi la Marekani CIA, na baadhi yao kuwahukumu kifo.

Askari wa kikosi cha ulinzi wa Jamhuri cha Iran wakijiandaa kuingia katika meli ya mafuta ya Uingereza kwenye mlango wa Hormuz.
Askari wa kikosi cha ulinzi wa Jamhuri cha Iran wakijiandaa kuingia katika meli ya mafuta ya Uingereza kwenye mlango wa Hormuz. HO / SEPAH NEWS / IRAN'S REVOLUTIONARY GUARDS WEBSITE/ AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo rais wa Marekani Donald Trump amekanusha madai hayo akisema kuwa taarifa za Iran kudai kuwa imewakamata majasusi 17 wanaofanya kazi katika Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, ni za uongo.

Trump amebainisha kuwa taarifa hizo ni za uongo na propaganda kama ilivyodai kuwa imeidungua ndege isiyokuwa na rubani.

Iran inasema kuwa majasusi wanaoaminiwa kufanyia kazi Marekani wamekamatwa katika kipindi cha miezi 12 hasi mwezi Marchi mwaka huu.

Wizara ya Intelijensia imesema kuwa washukiwa hao wamekuwa wakikusanya taarifa kuhusu mpango wa nyuklia, jeshi na sekta zingine nchini humo.

Baadhi ya majasusi hao walianguka katika ''mtego wa visa" uliyowekwa na CIA kwa raia wa Iran wanaotaka kusafiri nchini Marekani, Waziri wa intelijensia wa iran Mahmoud Alavi amesema.

Marekani na Iran zimekuwa zikizozana kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mvutano umeendelea kuongezeka kati ya nchi hizi mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.