Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-USALAMA

Washington yadai kuangusha ndege isiyo kuwa na rubani ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Javad Zarif amehakikisha kwamba hana taarifa kuhusu kutoweka kwa ndege isiyo kuwa na rubani, ambayo ilidunguliwa jana Alhamisi (Julai 18).Juni 20, Iran iliangusha ndege isiyo kuwa na rubani ya Marekani ambayo ilikuwa kwenye anga yake, kwa mujibu wa Tehran.

Meli ya Marekani, USS Boxer, katika Bahari ya Arabia kwenye picha iliyotolewa na jeshi la majini la Marekani Julai 14, 2019.
Meli ya Marekani, USS Boxer, katika Bahari ya Arabia kwenye picha iliyotolewa na jeshi la majini la Marekani Julai 14, 2019. Keypher STROMBECK / Navy Office of Information / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Marekani inasema kuwa imeangusha ndege isiyo kuwa na rubani ya Iran ambayo ilikuwa ikikaribia meli ya Marekani katika Mlango wa Hormuz.

Rais wa Marekani Donald Trump mwenyewe ametangaza kuwa Marekani imeangusha ndege hiyo ya Irani ambayo ilikuwa imekaribia meli ya Marekani kwa lengo la kuendesha shambulio, baada ya kupuuza wito uliotolewa mara kadhaa ili iondoke neo hilo.

Kwa mujibu wa rais Donald Trump ndege hiyo isiyo kuwa na rubani ya Marekani ilikaribia meli ya Marekani, USS Boxer, kwenye umbali wa mita 1,000 , ambayo ilichukuwa "hatua ya kujihami". "ndege hiyo iliharibiwa vibaya mara moja," amesema.

"Hakuna taarifa kuhusu ya kudunguliwa kwa ndege hiyo", kwa mujibu wa Tehran

Alipoulizwa muda mfupi baada ya kufika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jjini New York, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema "hanana taarifa kuhusu ya kuangushwa kwa ndege hiyo ambayo Marekani inadai kuwa ni ya Iran".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.