Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-VIETNAM-USHIRIKIANO

White Wouse: Hakuna mkataba uliofikiwa kati ya Trump na Kim

Ikulu ya Marekani, White House imesema kuwa hakuna makubaliano yaliyofikia mpaka sasa kati ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, katika mkutano wa Hanoi.

Rais wa Marekani amehakikishia kwamba "hakuwa na haraka" na alipendelea kufikia "mkataba mzuri".
Rais wa Marekani amehakikishia kwamba "hakuwa na haraka" na alipendelea kufikia "mkataba mzuri". REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House imebaini kwamba timu za viongozi hao zinatarajia kukutana tena baadaye, na mikutano yao imewezesha kuepo kwa mazungumzo mazuri na yenye kujenga, White House imesema Alhamisi wiki hii katika taarifa yake.

"Viongozi hao wawili wamezungumzia njia za kuendeleza mchakato wa kuachana na silaha za nyulia na mpango kuhusu uchumi," msemaji wa White House, Sarah Sanders, amesema.

"Hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa, lakini timu zao (za viongozi wawili) zinatarajia kukutana tena katika siku zijazo," Sarah Sanders ameongeza.

Donald Trump anatarajia kukutana na waandishi wa habari katika saa zijazo.

Mkutano huu ni wa pili kati ya viongozi hawa wawili, baada ya ule wa Singapore Juni 12, 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.