Pata taarifa kuu
IRAN-EU-USHIRIKIANO

Umoja wa Ulaya kuweka taasisi ya kisheria kwa kudumisha biashara na Iran

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa nchi wanachama utaweka mfumo mpya wa malipo ili kuruhusu kampuni za mafuta na wafanyibiahasra wengine kuendelea kufanya biashara nchini Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Zarif (wa pili kutoka kushoto) akizungukwa (kutoka kushoto kwenda kulia) na Federica Mogherini, Mkuu wa sera  za mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya, na wenzanke kutoka Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, Brussels Mei 15.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Zarif (wa pili kutoka kushoto) akizungukwa (kutoka kushoto kwenda kulia) na Federica Mogherini, Mkuu wa sera za mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya, na wenzanke kutoka Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, Brussels Mei 15. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limetolewa na Federica Mogherini, Mkuu wa sera anayeshughulikia mambo ya nje ya Umoja huo, lengo likiwa ni kuisaidia Iran kupeuka vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani baada ya kujiondoa kwenye mradi wa nyuklia.

Mpango wa nyuklia ulisainiwa mwaka 2015 kati ya Iran na        Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, Ujerumani na China.

Nchi hizo zilikubaliana kutoa vikwazo vya kiuchumi kwa mpango wa nyuklia wa Iran.

Hata hivyo toka Novemba 2016, Trump amekuwa akisema kuwa ataiondoa Marekani kutoka katika mpango huo usiokuwa na maana.

Viongozi wa mataifa ya magharibi wanasema kuwa wataendelea kuuunga mkono makubaliano ya kinyuklia ya Iran.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinasema kuwa watafanya kazi pamoja na matiafa yote yaliosalia katika mkataba huo huku ikiitaka Marekani kutovuruga utekelezwaji wake.

Mataifa mengine yalioweka mkataba huo wa mwaka 2015- Urusi na China pia yamesema yataendelea kuunga mkono makubaliano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.