Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-UHUSIANO

Korea Kaskazini na Kusini zakubaliana kuanza ushirikiano mpya

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wamesaini makubaliano mbalimbali ya kusaidia kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akiwa katika mkutano na mwenyeji wake, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un jijini Pyongyang, Septemba  18, 2018.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akiwa katika mkutano na mwenyeji wake, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un jijini Pyongyang, Septemba 18, 2018. Pyeongyang Press Corps/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa makubaliano hayo ni pamoja na namna ya Korea Kaskazini kuachana kabisa na mradi wake wa nyuklia, ambao umeendelea kutishia usalama wa Korea Kusini.

Korea Kaskazini pia imekubali kuachaana na majaribio ya makombora yake, ambayo yamekuwa yakionekana kutishia usalama wa Korea Kusini.

Kiongozi wa Korea Kaskazini amesema anatarajia kuzuru Korea Kusini hivi karibuni.

Mkutano huu umefuata ule uliofanyika mwezi Juni, baada ya viongozi hao wawili kukutana mpakani, lakini pia Kim Jong Un kukutana na rais wa Marekani nchini Singapore.

Kukutana kwa viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini, kumeleta matumaini ya kuimarika tena kwa uhusiano kati ya nchi hizo jirani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.