Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yatishia kufuta mkutano wake na Marekani

Korea Kaskazini imetishia kufuta mkutano na Marekani kufuatia mazoezi ya kijeshi  yanayoendelea  baina ya Marekani na Korea Kusini. Marekani kwa upande wake imefahamisha kwamba inaendelea na maandalizi ya mkutano huo.

Mkutano kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini ulipangwa kufanyika Juni 12 huko Singapore.
Mkutano kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini ulipangwa kufanyika Juni 12 huko Singapore. REUTERS/Kevin Lamarque, KCNA/Handout via REUTERS/File
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limesema kwamba mazoezi hayo ya kijeshi ni "uchokozi" na maandalizi ya uvamizi, jambo linaloashiria kurejelewa kwa lugha kali iliyokuwa inatumiwa wakati wa uhasama kati ya Marekani na Korea Kusini

Korea Kaskazini imetoa taarifa yake kuwa huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump kama Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia.

Mkutano huo utakao fanyika kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni.

Bw Kim amesema Korea Kaskazini "ilikuwa na matumaini makubwa kwamba mkutano huo ungechangia kupunguza wasiwasi katika Rasi ya Korea na kuwa hatua muhimu katika kuunda siku za usoni zenye matumaini makubwa.

"Inasikitisha sana kwamba Marekani inatuchokoza kabla ya mkutano huo kwa kutoa matamko ya kushangaza, " amesema Kim Jong-un.

Korea Kaskazini ilijiondoa ikisema imekerwa na mazoezi makubwa ya kijeshi yanayoandaliwa kati ya Korea Kusini na Marekani.

Mazoezi hayo ya kijeshi, yaliyopewa jina Max Thunder yalitarajiwa kufanyika katika kipindi ambacho michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ilikuwa inafanyika, lakini yakaahirishwa baada ya matumaini ya kuimarika kwa uhusiano kati ya Korea Kusini na Kaskazini kutokea.

Korea Kaskazini imefuta mkutano wake na Korea Kusini uliokuwa unatarajiwa pia kufanyika Jumatano  Mei 16 kufuatia mazoezi hayo ya kijeshi kwa ushirikiano na Marekani.

Maafisa wa ngazi ya juu wa mataifa hayo walitarajiwa kukutana katika eneo la mpakani ambapo majeshi hayaruhusiwi kujadiliana maelezo zaidi kuhusu makubaliano ambayo yalikuwa yameafikiwa katika mkutano mkuu kati ya mataifa hayo mwezi uliopita.

Awali Rais wa Marekani Donald Trump alisema, iwapo mazungumzo kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, hayataonekana kuzaa matunda atajiondoa.

Aidha, alisema kumekuwa na shinikizo za kutosha kuhakikisha kuwa Korea Kaskazini inaachana na mradi wake wa nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.