Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-MAREKANI

Korea Kusini yatilia shaka mazungumzo na Korea Kaskazini, Trump ana matumaini

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini , Kim Jong Un ana nia ya dhati ya kuja katika meza ya mazungumzo na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in.

Kiongozi wa Korea Kaskazini  Kim Jong  akiwa na mjumbe wa Korea Kusini baada ya kukutana hivi karibuni.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong akiwa na mjumbe wa Korea Kusini baada ya kukutana hivi karibuni. KCNA/via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya ujumbe wa Korea Kusini kuzuru Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong Un.

Imekubaliwa kuwa viongozi hao wawili watakutana katika mpaka wa nchi hizo mbili, huku ajenda kubwa ikiwa ni kujadiliana kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini ambao umeendelea kutishia usalama wa Korea Kusini.

Hata hivyo, rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema ni mapema sana kuwa na matumaini ya kufanyika kwa mazungumzo hayo ambayo pia yataishirikisha Marekani.

Aidha, amekanusha kuwepo kwa mazungumzo ya pembeni na Korea Kaskazini ili kufikia mwafaka wa kufanyika kwa mazungumzo hayo kuhusu mradi wake wa nyuklia unaotishia usalama wake na dunia.

"Hakuna mazungumzo yoyote ya pembeni yaliyofanyika kabla ya mwafaka wa kuwepo kwa mazungumzo haya," alisema rais Moon.

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa ni muhimu sana kwa Marekani kuhusika katika mazungumzo yoyote ili kupata mwafaka wa muda mrefu.

"Hatuwezi kupata amani ya kudumu kati ya mazungumzo ya Wakorea pekee," alisema rais Moon.

Uwezekano wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya nchi hizi mbili ulianza kuonekana baada ya Korea Kusini kuruhusu wanamichezo wa Korea Kaskazini kuhudhuria michezo ya Olimpiki yanayofanyika wakati wa msimu wa baridi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.