Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Michezo ya Olimpiki: Korea ya Kaskazini kutuma ujumbe wa watu 550 Korea Kusini

Korea Kaskazini imekubali kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi katika mji wa Pyeongchang, nchini Korea Kusini. Mashindano hayo yatazinduliwa Februari 9.

Korea Kaskazini na Korea Kusini wamekubaliana kuunda timu moja ya wasicahana itakayoshiriki mashindano ya Hockey.
Korea Kaskazini na Korea Kusini wamekubaliana kuunda timu moja ya wasicahana itakayoshiriki mashindano ya Hockey. AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Tayari Korea zote mbili zimekubaliana kufanya pamoja gwaride siku hiyo ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki.

Pia Korea kaskazini na Korea Kusini zimekubaliana kuunda kikosi kimoja katika mashindano ya wanawake ya Hockey.

Ujumbe wa Pyongyang utakuwa na wasichana wengi (230) na wasanii.

Awali Korea Kaskazini ilikua imependekeza kutuma wasichana zaidi ya 200 katika Michezo ya Olimpiki na kushiriki katika michezo ya wanariadha walemavu.

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilikubali kutuma ujumbe unaojumuisha wanariadha, maafisa waandamizi na wasanii katika mashindano ya Olimpiki ambayo yatazinduliwa tarehe 9 Februari katika mji wa Pyeongchang.

Seoul ilitafuta kwa muda mrefu kuonesha tukio hili kama "Michezo ya Amani" katika mazingira ya uhasama kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini na majaribio ya kombora ya masafa marefu.

"Uhusiano kati ya Korea mbili yalikua si mazuri kwa karibu miaka 10," alisema kiongozi wa ujumbe wa Korea Kaskazini katika mazungumzo hayo, Jon Jong-Su. Mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini yanafanyika katika mji Panmunjom, ulio kwenye mpaka kati ya Korea mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.