Pata taarifa kuu
BURMA-BANGLADESH-WAKIMBIZI

Burma na Bangladeshi wakubaliana kuwarejesha nyumbani Warohingya

Burma na Bangladesh wamekubaliana kwamba kwa kipindi cha miaka miwili watakua wamewarejesha wakimbizi 650,000 wa Rohingyas ambao wameitoroka Burma tangu mwisho mwa mwezi Agosti, wakimbia kampeni ya ukandamizaji ya jeshi la nchi hiyo.

Watoto, wakimbizi wa Rohingya wanasubiri kupewa chakula katika kambi ya Thankhali, Januari 12, 2018 Bangladesh.
Watoto, wakimbizi wa Rohingya wanasubiri kupewa chakula katika kambi ya Thankhali, Januari 12, 2018 Bangladesh. AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zimefikia mkataba huo katika mji mkuu wa Burma, Naypyidaw, "kuhusu hati ambayo itajazwa" wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Bangladesh imesema.

Hakuna kalenda ambayo imekua imewekwa mpaka sasana nchi hizo mbili.

Kwa upande wa Umoja wa Mataifa, unasema jamii ya Waislamu ya watu wachache waliathirika na "ukandamizaji wa kikabila".

Chini ya shinikizo la kimataifa, Burma iliahidi kuwarejesha nyumbani wakimbizi kama kweli watathibitisha kwamba walikua wakiishi Burma.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Bangladesh, makambi matano yatajengwa katika Jimbo la Rakhine, magharibi mwa Burma, ambapo wengi wa watu kutoka jamii ya Rohingyas waliishi.

Bangladesh, ambayo inawapa hifadhi karibu milioni moja ya wakimbizi wa Rohingya upande wa kusini-mashariki, katika kambi ambayo kwa sasa inachukuliwa kama kambi kubwa zaidi ulimwenguni, imekua ikihimiza serikali ya Burma ya Aung San Suu Kyi kuzindua mchakato wa kuwarejesha nyumbani wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.