Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Kim Jong-un aagiza kurejesha upya mawasiliano na Seoul

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameamuru kurejesha mawasiliano na Korea Kusini ili kujadili utaratibu wa mazungumzo kati ya Korea hizo mbili, afisa wa Korea Kaskazini amesema katika taarifa iliyosomwa leo Jumatano. kwenye televisheni ya serikali.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amjibu Donald Trump baada ya rais huyo wa MArekani kuitisha Kora Kaskazini kwamba ataisambaratisha.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amjibu Donald Trump baada ya rais huyo wa MArekani kuitisha Kora Kaskazini kwamba ataisambaratisha. KCNA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Njia pekee ya mawasiliano kati ya Korea mbili, "simu nyekundu", iliyokatwa mwaka 2013 kwa uamuzu wa Pyongyang, itaanza kufanya kazi kuanzia saa 06:30 (saa za kimataifa) leo Jumatano, alisema afisa huyo.

Tangazo hili linakuja baada ya pendekezo la rais wa Korea Kusini Moon Jae-in la kufanyika kwa mazungumzo ya ngazi ya juu tarehe 9 Januari ili kuandaa ujio wa wajumbe wa Korea Kaskazini kuhudhuria Michezo ya Olimpiki katika majira ya baridi mjini Pyeongchang nchini Korea Kusini, itakayoanza mnamo mwezi Februari.

Kurejeshwa kwa mawasiliano ya "simu nyekundu" ni "maendeleo makubwa", amesema leo Jumatano msemaji wa rais wa Korea Kusini.

Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya siku ya Jumatatu rais wa Korea Kaskazini alisem ayuko tayari kuzungumza na Korea Kusini, huku akiitishia Marekanikujibu kwa silaha za nyuklia ikiwa itaishambulia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.